WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya
Rais–Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete,
amewataka walimu wa shule za msingi na sekondari kutekeleza majukumu
yao kwa uadilifu na weledi lengo ikiwa ni kuweza kuzalisha wanafunzi
wenye ujuzi na maarifa ambao watalisaidia Taifa katika nyanja mbali
mbali.
Ridhiwani ameyabainisha hayo alipokuwa mgeni rasmi kwa
niaba ya Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, wakati wa
sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya Taasisi ya Shajar
ambayo inamiliki shule ya Baobab iliyopo Wilaya ya Bagamoyo.
Amesema
kwamba katika Taifa la Tanzania walimu wa shule za msingi na sekondari
wana mchango mkubwa sana hivyo wanapaswa kufanya kazi zao katika misingi
imara ambayo itaweza kusaidia kupata wataalamu bora.
Pia
Ridhiwani amesema ameridhishwa na ubunifu unaofanywa na wanafunzi wa
shule hiyo na kusisitiza kuwa kazi zao wanazozifanya kulindwa na
kusajiliwa.
Amesema kwamba uongozi wa Taasisi hiyo wanapaswa
kuwa daraja linalowavusha vijana kutoka kwenye vipaji kwenda kwenye
uzalishaji, huku wanafunzi wakifundishwa ufundi pamoja na ujasiriamali,
usimamizi wa fedha.
Katika maadhimisho hayo, Ridhiwani pia
amezindua Baobab Institute of Tanzania (BIT), akisema taasisi hiyo
haipaswi kuwa chuo kinachofuata mabadiliko ya dunia pekee, bali iwe
taasisi inayotafsiri mahitaji ya Tanzania ya leo na kesho pamoja na
Afrika.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Taasisi ya Shajar ambayo pia ndio wamiliki wa shule ya Bao Shani Swai,amebainisha
kwamba kwa sasa shule hiyo ina zaidi ya wanafunzi 1,000 na tangu mwaka
2007 hadi 2026, jumla ya wanafunzi wa 4,495 wa kidato cha sita
wamehitimu, huku asilimia 98 wakiendelea na elimu ya vyuo vikuu ndani na
nje ya nchi.
Shani ameeleza Taasisi hiyo ina miliki kituo cha
kulea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu, hospitali inayotoa
huduma za afya pamoja na shule za awali, msingi, sekondari na ufundi
stadi.
Naye Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Dkt. Lyabwene Mtahabwa, amewataka Watanzania kushikamana
katika kuwalinda watoto na kuhakikisha wanakua katika mazingira ambayo
ni rafiki na salama
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Shaibu Ndemanga
ameipongeza Taasisi hiyo kwa kuweza kushirikiana bega kwa bega na
serikali katika nyanja zote ikiwemo suala la kudumisha hali ya ulinzi na
usalama na shughuli za kimaendeleo.
Maadhimisho ya kilele cha
sherehe za miaka 20 ya Baobab yamehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa
serikali,vingozi wa tasisisi wezeshi,vingozi wa dini,wasanii pamoja na
wageni wengine kutoka maeneo mbali mbali.
NEMC YAANGAZIA UHIFADHI WA MAZINGIRA KATIKA KONGAMANO LA UCHUMI WA BULUU
-
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), katika
Kongamano la 5 la Kimataifa la Uchumi wa Buluu, limejipambanua katika sekta
ya mazing...

0 Comments