Mkuu wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Frank Nkinda amesema hayo leo alipokuwa akifungua jukwaa la vijana la halmashauri ya Msalala lililofanyika kata ya Bulyanhulu lililokusanya vijana zaidi ya 250 ambapo aliwaeleza mafanikio yoyote kila kijana anatakiwa asimame vizuri ili afikie malengo jambo kubwa ni kuwa na maono yako mwenyewe yenye kujenga.
Nkinda amesema malezi kwenye jamii bado ni changamoto kwani baadhi ya wazazi hawatoi malezi bora kwa watoto wanawaachia wajilee wenyewe wakati mwingine kuwatelekeza kwa bibi zao nakukosa malezi stahiki.“Familia nyingi zinahalibiwa na wazazi na sasa wapo watoto wanaojilea wenyewe utakuta mtoto wa miaka 17 amepanga chumba wakati mwingine anaishi na wadogo zake pekee changamoto hii ndiyo inachangia kuua ndoto za vijana wengi na kukosa uadilifu,uzalendo na hofu ya mungu”amesema Nkinda..
“Unaamini kijana mwenzangu Tanzania ya kesho ni mimi na wewe hivyo tuilinde kwa amani na upendo nakutumia vizuri simu zetu za mkononi kupata fursa za kimaendeleo”alisema Nkinda.
Nkinda amewaeleza serikali inataka kuona vijana waanze kuona maono yake kama wako shuleni watengeneza kupenda masomo ya sayansi wawe daktari, masomo ya sanaa wawe viongozi,masomo ya fedha hakika wakifanya vizuri watashikwa mkono nakufika mbali hayo ndiyo maono yanayotakiwa kwa nchi ya leo.
Nkinda amesema vijana waanze kufahamu fedha zilizotengwa na serikali kupitia wizara ya vijana na zile ambazo zinatengwa kwenye halmashauri ili waweze kufuatilia na kukopesheka kuliko kila kukicha kwenye mitandao ya kijamii kutoa lugha chafu na kuona picha gani imewekwa au mtu maarufu kaweka nini.
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Rose Manumba amema vijana kukutana hapa ni fursa pia kwani wanaweza kubadilishana mawazo na kuendelea kuwa wazalendo kwani kila kijana anao mchango wake wa kuijenga nchi,
Ofisa vijana kutoka halmashauri ya Bariadi ambaye alikuwa mwezeshaji kwenye jukwaa hilo Godwin Misana alisema uadilifu ni suala la msingi hata kama una kiu ya nmna gani lazima utangulize mbele uzalendo kwani wapo waliokuwa wakifanya kazi vizuri,wanafaulu mitihani yao vizuri darasani lakini huna hivyo ni kazi bure.“Vijana tutumie vizuri mitandao ya kijamii na matumizi ya simu yanaweza kuwa mabaya au mazuri inategemea wapo baadhi vijana wamekuwa wakitukana kwa kujibadilisha majina lakini wanasahau wanarudi kwa majina yao halisi nakuomba kazi hapo unajidanganya”amesema Misana.






0 Comments