Na Mwandishi wetu, Sumbawanga
WANANCHI wa kijiji cha Ng'ongo kata ya Mtowisa wilayani Sumbawanga wameiomba serikali kuwajengea nyumba watumishi wa Afya na kuongeza wahudumu katika Zahanati ya kijiji hicho huku Zahanati hiyo ikiwa na wahudumu wawili wote wakiwa ni wauguzi hali inayohatarisha Afya za wakazi wa eneo hilo.
Akijibu ombi hilo kwa wananchi Waziri wa katiba na sheria Juma Homera aliwahakikishia wakazi wa eneo hilo kuwa changamoto hiyo itakwenda kutatuliwa kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo pamoja na wananchi huku waziri huyo akichangia mifuko 100 ya saruji ili kuanza kwa ujenzi wa nyumba ya watumishi wa Afya na kuimarisha huduma za matibabu katika Zahanati hiyo.Waziri wa katiba na sheria Juma Homera amefungua Zahanati ya kijiji cha Ng'ongo iliyogharim Milioni 120 ikiwa Zahanati hiyo ilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi kwa milioni 20 huku serikali ikikamilisha ujenzi huo kwa sh. milioni 100.



0 Comments