Na Kareny Masasy,Shinyanga
USAFIRISHAJI haramu wa binadamu (TIP) umekuwa ni moja ya changamoto inayosumbua wasichana kutoka maeneo ya vijijini kwenda mjini kwa ahadi za kupatiwa ajira,elimu au maisha bora na baadaye wanaishia katika mazingira ya unyonywaji na unyanyassji.
Hayo yamesemwa leo na kaimu katibu tawala mkoa wa Shinyanga ambaye ni Ofisa Maendeleo ya Jamii mkoa Rehema Edson alipokuwa mgeni rasmi katika semina ya mafunzo juu ya Usafirishaji haramu wa binadamu na uhamiaji salama kwa maafisa wa serikali katika mradi wa emPoWeReD II .
Mradi huo unaotekelezwa na shirika la CVM and APA Kwa ushirikiano wa Chama cha Wafanyakazi wa Hifadhi,Mahoteli,Majumbani,huduma za jamii na Ushauri (Chodawu) pamoja na shirika la Wote sawa kwa kufadhiliwa na shirika la Kimataifa la Italian Agency for Development Cooperation.
Edson amesema kwa bahati mbaya watoto wengi hususani wasichana balehe ambao walitakiwa kuwa shuleni huishia kudanganywa kwa kusafirishwa kufanya kazi za nyumbani katika nyumba binafsi ambapo hukumbana na changamoto nyingi.
“Changamoto wanazokumbana nazo mojawapo ni masaa mengi ya kufanya kazi bila mapumziko,malipo duni au kutolipwa kabisa,kunyimwa haki ya elimu,unyanyasaji wa kimwili na kisaikolojia na unyonywaji wa kiuchumi”amesema Edson.
Edson amesema changamoto hii ni kubwa zaidi kwa sababu kazi za majumbani binafsi zinawafanya waathirika kuwa wagumu kutambulika kwa haraka ikiwa pia wamekuwa wakishuhudia aina nyingine ya ajira za watoto kufanya kazi mashambani,shughuli za ufugaji,uchimbaji mdogo wa madini, biashara zisizo rasmi na uuzaji wa bidhaa mitaani.
“Wahalifu wa sasa wamebadilisha mbinu hawategemei tena madalali wa kawaida pekee wanatumia tecknolojia,mitandano ya kijamii, matangazo ya ajira ya uongo na mifumo isiyo rasmi ya uajiri”amesema Edson .
Mwezeshaji kutoka. shirika la CVM Mwajuma Ally amesema Mradi huu umeanza awamu ya pili baada ya kuonekana mafanikio makubwa na utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2026 ambao umelenga hasa kwa wasichana na kuangalia wasichana wa kazi za nyumbani kuweza kujiendeleza kupitia vyuo vya mafunzoi na kupewa mikataba ya ajira na waajiri wao.
Mwezeshaji wa semina hiyo kutoka wizara ya mambo ya Ndani Providence Simbila amesema usafirishaji haramu wa binadamu ni kosa la kisheria kwa mujibu wa sheria zilizopo ndani ya nchi ya Tanzania na anayefanya kazi ya usafirishaji huo anakuwa na viashiria vya mambo matatu ambavyo vinaweza kubainika.
" Mambo hayo mojawapo ni matendo yanayotumika kumfanya akubali kusafirishwa, Mbinu za ahadi ya uongo kama mshahara mzuri na kazi nzuri ya muda mfupi ,Vitisho kwa lengo la kwenda kumfanyia kazi na kumnufaisha” amesema Simbila.





.png)
.png)


0 Comments