WAZIRI wa Madini, Mheshimiwa Anthony Peter Mavunde amesisitiza na kuwataka wawekezaji wote wa miradi ya uchimbaji madini kuanza utekelezaji wa miradi hiyo haraka ili kuchochea ukuaji wa sekta na pato la Taifa nchini.
Ameyasema
hayo leo tarehe 19 Juni, 2026 katika Ofisi ndogo za Wizara ya Madini
Jijini Dar es Salaam alipokutana na uongozi wa Kampuni ya Faru Graphite
Corporation ambao wapo mbioni kuanza utekelezaji wa mradi wa uchimbaji
madini kinywe Wilayani Mahenge, Mkoani Morogoro.
"*Mheshimiwa
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan* ameendelea kuwa kinara kwa kuweka
mazingira rafiki yanayovutia na kurahisisha uwekezaji nchini Tanzania.
Hili linaonekana wazi kwa miradi mingi ya wawekezaji iliyopo na ambayo
ipo mbioni kuanza utekelezaji wake"
Amesema
ni muda muafaka sasa kwa wawekezaji wote kwenye sekta ya madini ambao
miradi yao haijaanza utekelezaji kuunga mkono jitihada hizi za
Mheshimiwa Rais kwa vitendo na kuanza haraka utekelezaji wa miradi hiyo
ili ilete tija kwa Taifa.
Aidha,
Waziri Mavunde ametoa wito kwa uongozi wa Faru Graphite kuhakikisha
wanaharakisha kuanza utekelezaji wa mradi wao wa uchimbaji madini kinywe
Wilayani Mahenge ikiwa ni pamoja na ulipaji wa fidia kwa wananchi
wanaopisha utekelezaji wa mradi huo.
Waziri
Mavunde pia ameeleza kuwa, mradi huo mkubwa wa uchimbaji madini kinywe
utakaodumu kwa takribani miaka 26 utasaidia kuzalisha ajira na kuchochea
ukuaji wa uchumi wa Mkoa wa Morogoro na Taifa kwa ujumla.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Black Rock Limited, *Bw.
John De Vries* ameishukuru Serikali kwa namna inavyowapa ushirikiano
katika utekelezaji wa mradi huo na kuahidi kuwa Faru Graphite ipo tayari
kuendelea na kazi za awali za ujenzi wa mradi huo baada ya msimu wa
mvua kuisha ambao ulikuwa ni changamoto kwao.



0 Comments