SHIRIKA LA TCRS LIMEWEKA MIKAKATI YA UTUNZAJI MAZINGIRA KISHAPU


Na Kareny Masasy, Kishapu

SHIRIKA lisilokuwa la  kiserikali la  Tanganyika Christian Refugee Service (TCRS} limeweka mkakati wa utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti na kutoa elimu ya  matumizi ya jiko banifu kwa  lengo kukabiliana na  changamoto ya ukame iliyopo iliyopo wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga.

Hayo yamesemwa leo na  Mwezeshaji wa utunzaji wa mazingira kutoka shirika hilo   Emanuel Samweli kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yaliyofanyika Wilayani humo  kata ya Maganzo.

Samweli  amesema  kwa kufadhiliwa wa  kifedha kutoka Norwegian Church Aid (NCA ) wamekuwa wakitekeleza  mradi wa utawala bora,uhifadhi  wa chakula  na  kukabiliana na  mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kutunza mazingira kwenye kata  za Shagihilu,Bunambiu ,Ndoleleji na Bubiki.

Samweli amesema utunzaji wa mazingira wamekuwa wakiotesha   miti na kutumia njia ya matone kwa  kumwagilizia  na wajasiriamali kuwafundisha namna ya  kutumia majiko banifu.

“Tunawafundisha namna ya kutunza  visiki hai yaani miti  inayojiotea yenyewe na tunawafundisha namna ya kuitunza miti hiyo  ya asili na utumiaji wa bajiko banifu ikiwemo umwagiliaji wa kutumia matone”amesema  Samweli. 

 Ofisa Programu kutoka  NCA  Emanuel  Temu amesema wamekuwa wakishughulika  na utunzaji wa mazingira kutoa elimu na kuzijengea uwezo kamati za mazingira na klabu za shule za msingi  namna ya kukabiliana na majanga na upandaji miti.

  Temu amesema wito  ni wananchi kuendelea kutunza mazingira kwani  dira ya Maendeleo ya Taifa ya   2050 imeeleza   kuwajibika  na kutunza  mazingira  na ipo  mikoa 15 ya  Tanzania bara kwa kutekeleza miradi ya mazingira ikiwemo Shinyanga.

 Ofisa Mazingira kutoka  Halmashauri ya wilaya Kishapu Kassimu  Said amesema wamefanya usafi na zoezi la upandaji miti zaidi ya 300  kijiji cha Masagala  huku akisisitiza kuendelea kupanda miti na kuitunza kwani kishapu ni nusu jangwa.

“Makadirio ya upandaji miti ni milioni 1.5 na tunakimbizana na lengo la serikali inagawa utunzaji umekuwa changamoto angalau ifike robo tatu ya miti iliyostawi  kwa kupandwa”amesema  Said.

 


Diwani wa kata ya  Maganzo Hamza Tandiko  amesema   wana mradi wa maji yanaopatikana kwa asilimia 85 hivyo watajikita kupanda miti na kuimwagilizia ,mbolea ipo  na wanaotelekeza miti watachukuliwa hatua.



Post a Comment

0 Comments