
Na Kareny Masasy, Shinyanga

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita ameutambulisha rasmi mfumo huo leo nakuwaeleza waandishi wa habari kuwa hata kama mwananchi yeyote anataka kutoa taarifa zake kwa siri inawezekana kuna namna ambayo imewekwa kumlinda mtoa taarifa.
Hata ukitaka kutoa taarifa zako kwa siri usijulikane inawezekana na sio lazima utumie simu zenye mtandano hata zile ndogo zisizo na mtandao unaweza kutuma ujumbe bure ukapokelewa kwa namba maalum ya 0737108177.
Mhita amesema utaratibu wa kujiunga unaanza na nyota halafu namba 152 tena nyota na baadaye zero mbili na reli mwisho unaingia kwenye e-Mrejesho halafu unachagua na kuona mkoa wa Shinyanga kisha unatuma taarifa za pongezi,Ushauri na Malalamiko uliyonayo yatafanyiwa kazi.
“Kwa sasa tunatembea na kauli mbiu ya Sema Usikike na Mkuu wa mkoa na ofisi inapokea taarifa zote nakuzifanyia kazi kwenye e-Mrejesho na taarifa kama itahusika na taasisi fulani itapelekwa huko nakutolewa majibu kwa muhiska aliyetoa taarifa”amesema Mhita.
Mhita amesema mfumo huu umeanza muda kidogo ilikuwa bado wananchi wengi kuufahamu na leo sasa inatakiwa waufahamu ili wajue malalamiko yao,ushauri na pongezi zao zinakwenda wapi ili kufika kwa urahisi wakati mwingine wanaweza kutumia njia ya whasapp kwa namba hizo zilizotajwa
Mhita amesema kwa muda ulioanza wamepokea taarifa 25 na taarifa nne bado ziko kwenye uchunguzi hivyo amewataka wananchi hasa wenye malalamiko waweze kutumia mfumo huo ni rahisi kwao kupata majibu sababu kila siku asubuhi unafunguliwa na kusoma taarifa zote nakuzitolea majibu.
Mfumo huu unaenda kuondoa changamoto sababu lazima ulete mrejesho na faida zake utachagua ni njia gani utumie hata kama una usiri ni rahisi sana na unamlinda mtoa taarifa hata kama hatataja jina lake pia.
0 Comments