MALEZI YENYE MWITIKIO KWA WATOTO YANAHITAJIKA SANA KWENYE JAMII -SHINYANGA

Na Kareny Masasy, Shinyanga

SERIKALI mkoani Shinyanga  imewataka wadau kuwekeza zaidi katika malezi yenye mwitikio  huku ikipongeza hatua zilizofanywa na Halmashauri zote sita kuonyesha mafanikio kwenye  baadhi ya maeneo matano muhimu yaliyolengwa kwenye Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto.

Hayo yamesemwa na  Katibu tawala Msaidizi ambaye ni Mratibu wa chanjo Mkoa Timothy Sosoma  alipokuwa mgeni rasmi katika kikao cha  tathimini ya utekelezaji wa program hiyo kwa kipindi cha  miezi sita kuanzia mwezi Oktaba hadi Marchi kwa ufadhili wa  shirika la  Invest Children Society (ICS).

Sosoma amesema proramu hii ililenga maeneo matano ambayo kila mmoja wetu anapaswa kushiriki na serikali imeendelea kuwekeza zaidi  huku eneo la Malezi yenye mwitikio bado liko nyuma na ulinzi na usalama kwa watoto  sio kwa jeshi la polisi pekee ni watu wote.

Sosoma amesema jamii inatakiwa kurudi kama zamani mtoto wa mwenzio niwa kwako na leo wataona  kadi ya alama  kwa kuona picha halisi inayoongoza  ili kuwapeleka  kwenye utekelezaji zaidi na namna ya kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya malezi na makuzi.

 

‘Bila taarifa hatuwezi kujua nini kinaendelea hivyo ni muhimu kila halmashauri kueleza inatekeleza nini ili kuona wapi imefikia na kutenda bajeti ili kuwepo uendelevu wa usimamizi wa watoto na vituo vya kulea watoto vifanyiwe ukaguzi nakufuata utaratibu uliopo’amesema Sosoma.

 Afisa  Ustawi wa jamii mkoa wa Shinyanga Lyidia Kwesigabo akiongea kwa niaba ya Mganga mkuu wa Mkoa amesema ofisi ya mkuu wa mkoa  inaendelea kuratibu  Programu  ya  JPT-MMMAM kwa kushirikiana  na ICS ambalo ni kinara wa Malezi   na mwandishi kinara wa program hiyo  ambayo imelenga kuwezesha katika maeneo  matano  kuwa  ni Afya bora,Lishe,fursa za ujifunzaji ,Malezi yenye mwitikio na ulinzi na usalama.

Kwesigabo amesema mambo hayo yakitekelezwa kwa ujumuishi  yataongeza ukuaji timilifu  na  wenye tija kwa mtoto,familia na taifa  kwa ujumla.

Kwesigabo amesema katika maeneo hayo yote matano  yana viashiria  ambavyo  vinapaswa  kufikiwa  na huratibiwa  kupitia idara   na sekta  mbalimbali  ikiwemo  idara ya elimu, jeshi la polisi na sekta zinginezo.

 “ Bado  tunayokazi kubwa ya kuhakikisha  eneo la ulinzi wa mtoto na hasa  malezi yenye mwitikio  yanapewa nafasi kubwa kuanzia katika  upangaji wa  bajeti na utekelezaji wake kwa kushirikiana na wadau”amesema Kwesigabo.

Kwesigabo amesema kwa sasa kuna  kadi ya alama ya ECD  (Score card) iliyounganishwa  na mfumo  wa DHIS 2 ambayo inaonyesha viashiria mbalimbali  vya MMMAM ingawa  vipo viashiria vichache ambavyo havijaunganishwa katika kadi hiyo.

“Moja ya kipaumbele kilichopo ni kuanzisha maeneo ya kujifunia na kucheza watoto  (ECD corners) kwenye  mbalimbali ili kuweza kuleta uchangamshi  wa awali na ulinzi kwa mtoto ambapo amewaomba halmashauri  zote walipe kipaumbele suala hili  nakutoa elimu kwenye taasisi mbalimbali”amesema Kwesigabo.

 Ofisa  Programu kutoka   shirika la ICS Lucy  Mganga amesema wamekuwa wakitekeleza program za malezi na kupinga ukatili dhidi ya watoto wamekuwa wakishiriki program ya PJT-MMMAM  kwa kushirikiana na serikali tangu walipoanza mwaka 2023 na  leo wanaona mafanikio yaliyofikia  kwenye utkelezaji wa kipindi cha miezi sita.

“Tunatoa shukrani kwa Mtandao wa Malezi na Makuzi nchini  (TECDEN) kwa ushirikiano mkubwa na msaada wanaoutoa kwa kuhakikisha  kufikia malengo ya watoto kukua kwenye utimilifu wao.

 


Post a Comment

0 Comments