DC KAHAMA ATOA AGIZO NYUMBA ZA KULALA WAGENI KUONYESHA NIDA

 

                                          


                                        Na  Kareny  Masasy,Kahama

MKUU wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga  Frank Nkida ameanza kutekeleza agizo la kuwataka  wamiliki wa nyumba za kulala wageni  na wamiliki wa nyumba za kupangisha wahakikishe wateja wanaokuja wajiandikishe na kuonyesha kitambulisho cha Taifa (NIDA).

Ikiwezekana  wageni wakatoe taarifa kwa wenyeviti wa vijiji au mtaa ili kuondoa wimbi la watu kuingia bila taarifa na kuvunja sheria ikiwemo kuhatarisha hali ya usalama kama ilivyotokea mwaka jana mwezi Oktoba.

Mkuu wa Wilaya Nkinda amesema  hayo juzi  alipokuwa akiongea na wamiliki hao huku akiwaeleza lengo  la kuwaita ni kuimarisha hali ya usalama ya wilaya hii  kwa kushirikiana kwa pamoja nakutotaka hali ijirudie  tena.

“Tulikwisha kuta nyumba moja ina vijana 50 walioacha shule nakujiingiza kwenye vitendo viovu  lakini mmiliki wa nyumba hana wasiwasi wala kushtuka kutoa taarifa sehemu yoyote sasa ninataka kuimarisha ulinzi  kila mgeni anaeingia aonyeshe kitambulisho cha Taifa ni suala endelevu”amesema Nkinda.

Nkinda amesema imani iliyopo ni kukomesha vitendo vya kiuhalifu  na wanatarajia kufanya serikali ina macho   kwani amepokea maelekezo kutoka kwa waziri mkuu na kuhakikisha  maeneo yote yanakuwa salama hawategemei kuona watu wanakosa  utulivu katika kukuza uchumi wa kwenye kaya zao.

“Ni marufuku mgeni yeyote kuingia kwenye nyumba ya wageni kulala bila kujiandikisha  kila mmiliki ahakikishe awe na daftari lake na ukaguzi utafanyika atakaye kiuka atachukuliwa hatua”amesema   Nkinda.

Msimamizi wa vitambulisho vya Taifa wilayani Kahama Siriel Mchomvu  alisema  upo utaratibu wanaoufanya wa kutembea kwenye kila kijiji kuandikisha wanaohitaji vitambulisho na wale ambao hawajachukua kwenye  ofisi za kata ni vingi wajitokeze wakachukue.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama ambaye ni ofisa Tehama  Juma  Benjamin  amesema  kuna nyumba za kulala wageni zaidi ya 400 na wamiliki waliohudhuria ni wachache aliomba wakapeane taarifa hizi ili wakikutwa hawatekelezi wasilaumu watakapo chukuliwa hatua.

Mmiliki wa nyumba ya Wageni kutoka kata ya Kagongwa Suzana Kilaba ameeleza wananchi waishio vijijini wengi hawana vitambulisho vya taifa hivyo wanapokuja kwenye nyumba za wageni wasipewe huduma waliomba serikali hili suala waliangalie.


Post a Comment

0 Comments