LORI NA BUS YAGONGANA WATU SITA WAFARIKI DUNIA KAHAMA

 

Na  Mwandishi wetu,Kahama

WATU sita wamefariki dunia  na wengine watano kujeruhiwa  baada ya  Bus  la kampuni ya OJ  Classic  kugongana uso kwa uso na Lori  na kupinduka  katika kijiji cha  Wendere wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

 Kamanda wa jeshi la polisi mkoa Janeth Magomi  amethibitisha kutokea kwa ajali hilo leo majira ya saa 12.30 asubuhi  huku akieleza   Bus hilo lilikuwa likitokea Kahama  mkoani  Shinyanga  na lilipofika  eneo la Wendere ndipo lilipogongana  na lori  na  kwenda kupinduka.

Kamanda Magomi amesema   Bus hilo lenye namba za usajili  T985DXL aina ya TATA  mali ya kampuni ya OJ Classic  ambapo chanzo chake  kimebainika ni uzembe wa dereva wa basi hilo.

Kamanda Magomi amesema  ajali hiyo imesababisha watu sita kufariki  na majeruhi watano ambao walikuwa  wakisafiki kutoka Kahama kuelekea mkoani Geita,

“Walipofika  kijiji cha Wendere Dereva aliona gari lingine lililokuwa kati kati ya barabara  na Lori lilikuwa likija upande wake hakulipisha wala   kusimama ili  kulipisha na matokeo yake aligonga gema na matokeo kuanguka  upande wa kushoto ”amesema  kamanda   Magomi.

Hata hivyo kamanda  Magomi jeshi la polisi limeendelea kumtafuta dereva wa bus Chacha Bosco  (35)  ambaye alisababisha ajali hiyo nakufanikiwa kutoroka baada ya ajali  na dereva wa Lori alijeruhiwa vibaya.

Kamanda Magomi ametoa  wito kwa madereva kuchukua tahadhari   wakiwa barabarani ili  kuokoa ajali au vifo visivyo vya lazima.


Post a Comment

0 Comments