Mrajisi
Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga Ibrahim Kakozi amesema hayo juzi kwenye jukwaa la Maendeleo la ushirika lililofanyika mjini Kahama huku akieleza ushirika una
wanachama 28,000.
Kakozi amesema vyama vya ushirika vinaendelea kuwa na mali zenye thamani ya mabilioni ya fedha lakini bado kuna changamoto za upungufu wa watendaji, uelewa mdogo wa baadhi ya wanachama na udhaifu wa nidhamu ya mikopo.
Kakozi
ametoa wito wa kuimarishwa kwa matumizi
ya mifumo rasmi ya malipo badala ya fedha taslimu ili kuongeza uwazi na
kupunguza upotevu wa fedha katika minyororo ya biashara ya mazao.
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) Emanuel Nyambi amesema sekta ya ushirika Mkoa wa Shinyanga imeendelea kuwa chachu ya maendeleo kwa kuongeza ajira, masoko na kipato cha wakulima.
"Zaidi ya watu 25,000 wananufaika na ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kupitia shughuli za ushirika, zikiwemo uchakataji wa mazao, usafirishaji na masoko"amesema Nyambi.
Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro amesema ushirika ni nyenzo muhimu ya utekelezaji wa sera za maendeleo za Serikali katika kuinua uchumi wa wananchi hususan wakulima.
Mtatiro amesema Mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa maeneo yanayoongoza kwa uzalishaji wa pamba na tumbaku nchini huku akieleza kuwa mafanikio hayo yametokana na ushirikiano kati ya Serikali, vyama vya ushirika na wadau wa maendeleo.
Mtatiro amesema Serikali kupitia mfumo wa ushirika imeendelea kutoa ruzuku ya pembejeo ikiwemo mbolea na viuatilifu hatua iliyosaidia kupunguza gharama za uzalishaji na kuongeza tija kwa wakulima.

0 Comments