HALMASHAURI ya wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga imebaini kaya
5881 kutokuwa na vyoo ikiwa kaya 3335 zimejenga vyoo vya muda hali
ambayo inaonyesha kuwa hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko
hasa ya kuhara na kipindupindu.
Kaya hizo zilibainika wakati wa kampeni inayoendelea ya usafi wa
mazingira na kuihamasisha jamii kuwa na vyoo bora katika kata zote za wilaya
hiyo kwa kutumia sheria ndogo za halmashauri, huku mila na desturi
zikitajwa kuwa ni chanzo cha kuwepo tatizo hilo na kuona ni muhimu kwa kujisaidia
vichakani.
Akizungumza na waandishi wa habari afisa mazingira wa wilaya ya Kishapu Mohamed
Mlewa, alisema wilaya inakaya 42,000 kati ya hizo zenye vyoo bora ni 12,680 vya
kawaida 20,114 na ambavyo vimejengwa kwa matumizi ya muda ni 3335 huku
kaya 5881 vikiwa havina vyoo .
“Ni muhimu kila kaya iwe na choo tena tunasisitiza kiwe bora na ndiyo maana
tunaendelea kutoa elimu kwa jamii, iweze kubadilika iache mila na desturi
zilizopitwa na wakati kama sasa hivi tumebaini kuwepo kaya 5881
zisizokuwa na vyoo hata vya muda hawana”alisema Mlewa.
Alisema walitembelea kata za Masanga ,Shagihilu,Mwamashele na Ukenyenge
ambapo walizungumza na wananchi na kutoa elimu sanjari na kukagua kaya
kama zinavyoo nakukuta baadhi hazina ambazo walizitaka kuhakikisha wanachimba
haraka il kuzuia kuibuka magonjwa ya mlipuko.
Ameitaka jamii kubadilika kwa kuhakikisha mazingira wanayoishi yanakuwa
safi ,hatua itakayosaidia kujiepusha kukumbwa na kipindupindu hasa
kipindi hiki cha mvua za masika zinazoendelea kunyesha, ambapo hutokea mlipuko
wa magonjwa mbalimbali mazingira yakiwa machafu.
Wakati huo huo ilibainika pia kukosekana kwa miundombinu bora ya
maji na vyoo pamoja na mazingira machafu umesababisha nyumba za kulala wageni
tatu na hoteli mbili kufungwa, katika halmashauri hiyo.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya idara ya usafi wa mazingira wilayani humo
kufanya ukaguzi na kubaini kuwepo changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na
kukosekana kwa maji,kalo la maji machafu na miundombinu ya ndani kutoridhisha
yakiwemo mashuka hivyo kuhatarisha afya za wateja.
.“Hili zoezi lilifanyika march 27 mwaka huu katika mji wa mhunze ambapo
tulifunga hotel mbili na kisha mji mdogo wa Maganzo hoteli moja na nyumba
za kulala wageni mbili,tunaendelea na zoezi hili kwa wilaya nzima ili
kuhakikisha mazingira yote yanakuwa safi ”alisema Mlewa.
Afisa mazingira alisema zoezi hilo limeanza kwa kupitia hoteli na baa na kwamba
hatua itakayofuata ni kukagua migahawa,ambapo aliwataka wananchi
kuhakikisha wanaweka mazingira katika hali ya usafi ili kuzuia mlipuko wa
magonjwa ambao unaweza kutokea kwa kusababishwa na uchafu.
0 Comments