TAKUKURU SHINYANGA YAOKOA ZAIDI YA MILIONI 123.3 ZA POS NA UNUNUAJI ZAO LA PAMBA


TAASISI ya  Kuzuia na Kupambana na  Rushwa (Takukuru) Mkoani Shinyanga wamefanikiwa kuokoa zaidi ya Shilingi Milioni  123.3  kupitia ufuatiliaji kwenye ukusanyaji wa Mapato kwa njia ya Mashine ya Kielektroniki  (POS)  katika Mnada  wa Old Shinyanga na Ununuzi wa zao la pamba Kishapu  mwaka 2025/2026.

Naibu Mkuu wa Takukuru  Mkoa wa Shinyanga Mwamba Masanja amesema hayo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa  habari  huku akiwaeleza  mafanikio hayo ni kutoka kipindi cha kuanzia mwezi April  hadi  Septemba.

Masanja amesema  zaidi ya  shilingi   Milioni  75.5 zimetoka katika Mnada wa Old Shinyanga  uliopo Manispaa  ya Shinyanga ambazo hazikuwasilishwa benk kwa wakati kama inavyotakiwa.

"Baada ya Ufuatiliaji huo Takukuru ilibaini baadhi ya Mawakala wa  ukusanyaji Ushuru kupitia POS walibaki na fedha  hizo bila kuziwasilisha benk"amesema Masanja.

Wakati huo huo Masanja amesema  wamefanikiwa pia kuokoa zaidi ya Shilingi Milioni 47.7 kutoka kwenye matumizi ya fedha za ununuzi wa zao la pamba kwenye msimu wa mwaka 2025/2026 katika halmashauri ya wilaya ya Kishapu.

"Makampuni yenye kibali cha kununua pamba kwa msimu huo yalikabidhi fedha katika vyama vya msingi  vya ushirika  vya mazao (Amco's) kwaajili ya manunuzi ya pamba kwa wakulima"amesema Masanja.

Masanja amesema  baada ya ufuatiliaji huo  kutoka Takukuru ilisaidia wakulima kulipwa fedha zao.

Masanja amesema mikakati  inaendelea ya kuzuia rushwa katika robo ya pili ya mwaka kwa njia ya uelimishaji katika maeneo ya utoaji wa huduma na ufuatiliaji wa Matumizi ya fedha za umma katika miradi ya maendeleo.

mwisho.

Post a Comment

0 Comments