NSSF KAHAMA YAFUNGA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUJITAFAKARI



WIKI ya huduma kwa wateja  upande wa  Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeona ni fursa muhimu ya kutafakari  namna  ya kuwahudumiwa wateja ,kusikiliza mahitaji yao na kuendelea kuboresha  huduma.

Kaimu Meneja  wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii ( NSSF)  Kahama    Rama  Namwandu  amesema hayo leo  wakati wa kufunga  maadhimisho  ya wiki  ya huduma kwa wateja   huku yakiwa  na  Kauli mbiu  ‘HUDUMA BORA KWA VITENDO.

 “Mafanikio haya  yanaonyesha   juhudi zinazoendelea  za kuimarisha  mfuko wa kupanua wigo wa hifadhi ya jamii ikiwemo kuwafikia wananchi waliojiajiri  kupitia skimu ya hifadhi”amesema   Rama.

Rama  amesema    wanaendelea kuwafikia wananchi  waliojiajiri  na  wanaofanya shughuli  mbalimbali za kiuchumi ,kuwaelimisha  kuhusu umuhimu  wa hifadhi  ya jamii  na kuwahamasiha  kujiunga pia.

Rama  anawasihi wanachama kutumia huduma za kidijitali  za mfuko hususan katika kufungua na kufuatilia madai ya mafao yao kwa njia ya mtandao  ili kurahisisha  upatinajaji  wa huduma,  kuokoa  muda  na kupungua ulazima wa kufika katika ofisi za NSSF.

Ofisa Mafao kutoka NSSF Kahama  Albert Mbago anasema  wamekuwa wakitoa  huduma bora kwa vitendo nakuwaeleza wateja wote kuwa mfumo umeendelea kuboreshwa kwani   wanachama waliojiajiri  wahakikishe wanachangia kila mwezi na majina yao  yasomane  na vitambulisho vya taifa.

 Ofisa  kitengo cha Matekelezo  kutoka NSSF  Kahama  Magreth Mwaibasa   akiongea kwenye siku ya kufunga maadhimisho  ya wiki ya huduma kwa wateja  anasema  awali mfuko huo  ulikuwa unahusika na wateja walioajiriwa  serikalini pekee   lakini sasa yakaja mabadiliko   na maboresho.

 “ NSSF imejikita  kuwafikia   wajasiriamali  wote  ikiwa lengo kubwa  kuwafanya waweze kunufaika na mafao ya pensheni ya uzeeni  kama mtu aliyeajiriwa serikalini    atakapofikisha umri wa  miaka 55 na kuendelea”amesema Magreth 

Magreth  amesema   watu wote bila kuchagua wanahimizwa   wajiunge kuwa mwanachama wa mfuko huu kwani  masharti ya kuanza kunufaika ni pale atakapokuwa amechangia kwa kipindi cha miaka 15  ikiwa mfuko huo  upo  kwaajili ya maisha ya badaye.

 “Kitu ambacho mjasiriamali atapata shangwe ni kupata mafao ya matibabu   na  atapaswa kuchangia  kila mwezi  shilingi 30,000 bila kukoma  na mchanganuo wa fedha hizo  shilingi 10,000 itakwenda kwenye matibabu na  shilingi 20,000 itakwenda kwenye mfuko wake wa akiba”anasema  Magreth.

Magreth  amesema   waliokuwa wanachama wameanza kunufaika kwa kupata matibabu kulingana na masharti yaliyowekwa hivyo kama mwanachama  akitaka kuchangia shilingi 52,200 atanufaika  na familia yake  ya watu sita   ambapo shilingi 20,000  itakwenda  kwenye  mfuko wa akiba  yake




Post a Comment

0 Comments