MANISPAA YA KAHAMA KUISHIKA MKONO TAASISI YA HOLYSIMILE AMBAYO IMEJIKITA KUIBUWA MDAU SHUPAVU ALIYESAHAULIKA

 

         

TAASISI ya  Holysimile  kupitia jukwaa la Mdau  Shupavu Mkoani Shinyanga  limeahidiwa kushikwa mkono na Manispaa ya Kahama kwa kupatiwa shilingi Milioni kumi ili iendelee kusaidia  uhamasishaji wadau wa sekta mbalimbali  kutambulika na kujinyanyua kiuchumi.

Hayo yamesemwa leo na Ofisa Utamduni  Manispaa hiyo Mwaita Mwingimkuu  alipokuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa Masudi Kabetu  katika utolewaji wa tuzo za Mdau Shupvu kwa wadau walioshiriki katika vinyang’nyiro  mbalimbali  nakupata ushindi.

Mwinyimkuu amesema  taasisi hii imekuwa ikifanya kazi kubwa  katika uhamasishaji maendeleo ndani ya Manispaa ambapo watamshika mkono kwa kumuondolea pia vibali vyote nakuendesha shughuli hiyo bure.

‘Nilishiriki mashindano ya Miss Shinyanga wiki iliyopita  mgeni rasmi aliyekuwepo  ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu kwa niaba ya mkuu wa mkoa  Mboni Mhita alisisitiza kutenga bajeti kwenye idara ya utamaduni ili kusaidia  taasisi kama shupavu inayojitolea kufanya kitu kizuri  cha  kuleta elimu na maendeleo kwa jamii”amesema Mwinyimkuu.

 Mkurugenzi wa Taasisi  ya  Holysimile  kupitia jukwaa la  Mdau Shupavu  Arnold Gweichumu  amesema amekuwa mwanzilishi wa jukwaa la Mdau Shupavu kwa kanda ya ziwa na sasa atakwenda kuanzisha ngazi ya taifa kwani  wadau ngazi ya chini wamekuwa wakifanya kazi kubwa nakusahaulika hivyo ameamua kuwaibua kwa kuwapa tuzo waendelee kujithamini kwenye kazi zao.

“Ninashukuru mashindano haya niya wazi  mtu anapotaka kushiriki moja kwa moja anaruhusiwa anaona kura zinavyopigwa mtandaoni  kihalali kabisa  bila upendeleo  na ushindi unapatikana “amesema Bweichumu.

 Bweichumu amesema  anamshukuru mungu kwa washiriki kufika asilimia 90 ukumbini  nakuchukua tuzo zao  huku akishukuru wadau mbalimbali kuendelea kumuelewa polepole ambapo amekuwa wakitumia  njia ya kidijitali  kuhakikisha anakwenda na wakati.

 Wadau  walioshiriki tuzo mbalimbali ni zaidi ya 50 na kila kinyang’anyiro  kilikuwa na watu watatu mpaka wanne walikuwa wakishindana kwa  kupigiwa kura mtandaoni  na sekta ya madini ,mapambo, uandishi wa habari,mtangazaji bora wa redio,kituo bora cha redio, jukwaa la  redio la kijiditali, washereheshaji   wachenjuaji  na wauzaji  wa madini  pamoja na  sekta ya  utalii wamejitokeza zaidi. 

Emmanuel   Manoni aliyeshinda  upande wa  sekta ya utalii  amesema  ushiriki wa tuzo hizi yeye ni mara ya nne kwani zimempatia heshima kubwa katika uhifadhi na utunzaji wa mazingira huku mwandishi wa Habari Neema Nkumbi akielezea namna ambavyo tuzo hizo zimempatia ujasiri  ingawa mwanzoni alikuwa na hofu ya kushindwa. 

Post a Comment

0 Comments