MFUKO wa Taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) umejivunia mafanikio ya kuongeza idadi ya wanachama, kuboresha Mifumo ya Tehama huku ikieleza kuwafikia wananchi waliojiajiri kupitia skimu ya hifadhi.
Akiongea kwa Niaba ya Mkurugenzi wa NSSF nchini Meneja wa mfuko huo mkoa wa Kahama Rose Metta amesema hayo leo kwenye ufunguzi wa wiki ya huduma kwa wateja yakiwa na kauli mbiu ‘huduma bora kwa vitendo’ nakutoa vyeti vya pongezi kwa wateja wanaozingatia sheria kikamilifu.
Metta amesema wanaendelea kuwafikia wananchi waliojiajiri na wanaofanya shughuli mbalimbali za kiuchumi kuwaelimisha kuhusu umuhimu wa hifadhi ya jamii na kuwahamasisha kujiunga na mfuko huo ambapo lengo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kila mtanzania aweke mafao kwaajili ya matibabu na uzeeni.
“Maboresho haya yameendelea kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma na ulipaji wa mafao kwani wastani wa muda kulipa mafao umepungua kutoka siku 63 katika mwaka mwaka wa fedha ulioishia mwezi Juni 2021 hadi siku 19 katika mwaka wa fedha ulioishia 2025/2026”amesema Metta.
Metta amehimiza wanachama kuendelea kufuatilia taarifa zao NSSF na kutoa taarifa pale wanapoona changamoto au kutokuwepo kwa michango yao kwani ni muhimu kuhakikisha taarifa zao zinakuwa sahihi na kulinda haki zao za kupata mafao kwa wakati.
Mkuu wa idara ya Mafao kutoka NSSF kahama Albert Mbago amesema wamekuwa wakitoa huduma bora kwa vitendo huku akiwashukuru wateja wote na kuwaeleza mfumo unaendelea kuboreshwa kwani kuna wanachama wa hifadhi skimu au (wanajichangia binafsi) huduma yao inaendelea kutokewa vizuri
Akiongea kwa niaba ya wanachama wachangiaji binafsi Mchungaji Meshack Guranywa amesema huduma ya kuchangia kwenye mfuko huo kwa mara ya kwanza alianza mwaka 2020 nakuona umuhimu wake alipougua nakulazwa hospitalini nakutozwa gharama ya matibabu shilingi milioni tatu ambapo zilizolewa na mfuko huo








0 Comments