DIWANI KATA YA MJINI KAHAMA AIBUKA NAKUELEZA UKWELI KWENYE MAENEO YA WAFANYABIASHARA YASIYO RASMI

 

 

   

DIWANI  wa kata ya Kahama  Mjini  Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga  Godson  Andrew  ameibuka nakueleza zoezi kweli limeanza  ila  wafanyabiashara wadogo  wawe na subira   ili wajipange kwenda kwenye maeneo rasmi yaliyotengwa  na Halmashauri.

 Kutokana na taarifa iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassa  kuwa Halmashauri  zipange  miji na kuweka mazingira  safi  hilo ni jambo zuri .

Andrew amesema hayo leo  kufuatia  zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara wadogo walioweka bidhaa zao nakuanza kufanya  biashara  kiholela  eneo la kata ya mjini jambo ambalo ameliona nakuanza kulifanyia kazi kwa utaratibu  ulio mzuri uliopo ndani ya Halmashauri .

 Andrew  amesema  kupitia zoezi  la kuwaondoa kwenye maeneo yasiyo rasmi  ni utekelezaji wa  tahadhali ya taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA)  kuwa  kipindi cha  masika kutakuwa na  mvua  za kiwango cha juu hivyo ni wajibu  sasa wa kuweka mji safi nakusafisha na kuzibua  mitaro.

 “Tuzingatie suala la usafi na kuzibua mitaro  kwani kitengo cha mazingira cha Halmashauri   wamekuwa wakifanya jitihada mbalimbali  za kuzoa taka ngumu na kuzibua mitaro lengo kuweka mazingira safi ya ufanyaji biashara  na kujihami na mvua hizo”amesema Andrew.

Andrew amesema  tamko lililotolewa lengo lake ni watu wote  kujipanga na  wafanyabiashara wawe katika mazingira safi  hivyo kama kiongozi wanakubaliana na kuwepo ujasilimali au wafanyabishara wadogo  ambao wanaipatia  halmashauri  mapato.

Andrew amesema  wafanyabishara wadogo ndiyo wamebeba taswira   ya kata ya Mjini  wamekuwa wakijihusisha na uuzaji wa  bidhaa za matunda wengine kusukuma matolori kupeleka bidhaa  hivyo  wawe na subira wanaangaliwa kwa jicho la kipekee  yapo maeneo yaliyorasmishwa wao kukaa vizuri na kufanya biashara zao.

“Nashauri tukutane wadau wote tuzungumze ili kufikia hatua ya kuweka mji wetu safi tutajipanga vizuri kwani yapo maeneo ya wazi yaliyotengwa rasmi  sababu wanaiingizia halmashauri mapato nakukuza uchumi wao” amesema   Andrew.

Baadhi ya wafanyabishara wadogo   wamedai zoezi la kuondolewa limekuwa ni ghafla wameomba muda ili wajipange kuondoka maeneo hayo kwani hata matangazo hayakupita kuwapa taarifa.





Post a Comment

0 Comments