WALEZI NA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KULEA WATOTO WAJULISHWA KUITAMBUA PJT-MMMAM

Na Kareny Masasy, Shinyanga

WALEZI na wasimizi wa vituo vya kulea watoto wadogo Mchana (Daycare) Manispaa ya Shinyanga wametakiwa kutambua programu Jumuishi ya  Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto PJT-MMMAM  ili kuwaweka watoto kwenye ukuaji wenye utimilifu.

Hayo yamesemwa  na Ofisa Ustawi wa Jamii  kutoka Manispaa hiyo  Elizaberth Mweyo ambaye alikuwa mwezeshaji katika semina ya siku mbili  kwa walezi na wasimamizi hao zaidi ya 20 iliyoratibiwa na shirika lisilo la kiserikali la Invest to Children in the Society  (ICS)  kwa lengo la kuwajengea uwezo na utambuzi wa programu hiyo kwa umuhumu wake.

Mwenyo amesema  katika vituo wapo walezi wapya na wengine wazamani  hivyo wanatakiwa kutambua  PJT-MMMAM  na kuzingatia kundi la watoto wenye umri wa kuanzia miaka 0 hadi minane kwa utafiti uliofanyika watoto hao ubongo wao unaendelea kukua na hata kwenye vituo vya kulea watoto  mnao wenye kuanzia umri wa miaka miwili  hadi minne.

"Katika programu Jumuishi tunaangalia  nguzo tano muhimu ambazo zinamuwezesha mtoto kabla ya kuzaliwa na baada ili kuendelea kukua katika utimilifu wake ambavyo  ni lishe,afya bora,Malezi yenye Mwitikio.Ujifunzaji wa awali na ulinzi na usalama"amesema Mweyo.

Ofisa Ustawi wa jamii Mkoa wa Shinyanga  Lyidia Kwesigabo ambaye aliakuwa mwezeshaji katika mada ya huduma za ulinzi. na usalama  wa mtoto amesema  vipo viashiria vinavyoonyesha mtoto kufanyiwa vitendo vya ukatili na kituo lazima kiwe na kamati inayojumuisha wzazi na kisifsnye kazi zaidi ya masaa 12 wala kulaza watoto (boarding) .
Ofisa Programu kutoka Shirika la Invest  to Children in Society(ICS )Lucy Maganga amesema   katika utekelezaji huu wamekuwa waratibu  na kufanya mambo mawili ya kuimarisha mifumo  na uchechemuzi  na vituo vya kulea watoto ni mojawapo ya kujengewa uwezo.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Emmanuel Rueben  ambaye alikuwa mgeni rasmi akifungua semina hiyo amesema wanatambua vituo vinapokea watoto wenye umri wa miaka miwili hadi minne na  wana waandaa kiakili na kimwili  na ndiyo maana wanasisitizwa kuwapa lishe bora yenye makundi ya aina tano za vyakula.

Reuben amesisitiza kwenye maeneo ya vituo kuwepo mazingira  safi na salama, maeneo ya kupumzikia, matundu ya vyoo yenye uwiano ,kutambua umuhimu wa chanjo kwa watoto  na kuwaelimisha wazazi ikiwemo vituo kuvisajili kwa mujibu wa sheria,taratibu na miongozo.

Mwenyekiti wa vituo vya kulea watoto mchana  Manispaa ya Shinyanga  Damari Molles amesema  semina hiyo imekuwa ni fursa kwao kuongeza ubora kuleta ufanisi katika vituo kwa walezi na wasimamizi  kwa kuhakikisha watoto wanakua  kwenye hali nzuri.



Post a Comment

0 Comments