NABII SUGUYE AGUSWA NA WATOTO YATIMA KAHAMA ATOA MSAADA WA VYAKULA ,FEDHA ZA UJENZI WA UZIO

 
 
Na Kareny Masasy, Kahama

KIONGOZI wa dini  Nabii Nicolaus  Suguye   ameguswa kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo unga na sukari kwa watoto yatima wanaoishi kwenye vituo viwili vya Hope na  Peace vilivyopo kata ya Zongomela  Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga

Suguye ametoa msaada huo leo  kwa nyakati  tofauti   ambapo amesema kabla ya kuanza mkutano wa injili  ameamua kuwashirikisha kundi hilo kuwapa zawadi  ili wasijione kama wapo peke yao  ikiwa wao watambue  ndiyo wazazi wao kwa sasa.

Suguye  amesema amesikiliza changamoto mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na walezi wa vituo hivyo   mojawapo kituo cha Peace kukosa uzio nakuwafanya watoto  wakati mwingine kupotea hilo amelichukua nakulifanyia maamuzi papo  hapo.

“Leo nimekuja hapa kuwasaidia watoto yatima sio kujionyesha  kwani wanamahitaji  mblimbali  muhimu na jambo hili tunalifanya kwa kukutanika  na mungu  nakuweka  baraka zake  kitabu cha mungu (bibilia) kinasema  saidia wajane na yatima  bila ubaguzi  kwani wote ni wa mungu”anasema Nabii  Suguye.

 Nabii Suguye  amewataka watoto hao kutojiona wanyonge  siku zote kwani mungu ndiye  baba wa watu wote na siku zote hawezi kuwaacha kama alivyobinadamu.

  Nabii Suguye  ameguswa  na maamuzi ambayo ameyatoa kwa haraka ni  kutoa shilingi Milioni tatu sawa na matofali 3000  na mifuko  50 ya saruji  kwaajili ya ujenzi wa  uzio ili kuwaondole changamoto iliyoelezwa na msimamizi wa kituo hicho.

Msimamizi wa  kituo cha  Peace Opharn  Abubakar Issa  amesema kituo hicho kilianzishwa mwaka 2004 na kimekuwa kikilea  watoto yatima  na  mpaka sasa kuna watoto  93 ambapo  wakiume  ni 43 na wakike ni  50 na pia wanalea watoto waliochini ya umri wa miaka mitano wanahitaji maziwa kwa wingi changamoto kubwa ni kukosa uzio  unaowafanya baadhi ya  watoto kupotea au kuumwa na mbwa wanao zulula hovyo mitaani.

“Nimeshukuru sana kwa msaada huu kwa kuguswa  huko muendako mkawe mabalozi wazuri  kutangaza kituo hiki ili wadau wengine waguswe kuja kutoa msaada  nanimefurahi sana  kiongozi Suguye  kuguswa  na ujenzi utaanza mara moja kwani  tayari  mafundi walikwisha fanya tathimini mahitaji yake mpaka kukamilika”amesema Abubakar

Msimamizi wa kituo cha hope  Scholastika  Fred amesema kituo kilianzishwa mwaka 2022 kina watoto zaidi ya 100 kinajihusisha na malezi ya watoto na  mahitaji ni chakula  na ada kwani wapo wanaosoma  chuo cha ufundi stadi (veta) ambapo lishukuru kwa msaada uliotolewa wa mahitaji muhimu kwao.


Post a Comment

0 Comments