WADAU MKOANI SHINYANGA WAUNDA KIKOSI KAZI KUPAMBANA NA WASAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU



:
WADAU mbalimbali  mkoani Shinyanga  wameunda kikosi kazi cha kupambana na usafirishaji  haramu wa binadamu ( ATS) nakuandaa mpango kazi kwa kipindi cha mwaka  mmoja ambao utajumuisha utoaji wa elimu kwenye jamii kwa lengo la kuthibiti usafirishaji huo.
Mrakimu mwandamizi  wa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga Issa Kisiroti ambaye amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kikosi kazi hicho  amesema   hayo LEO  baada ya kukamilisha  mpango kazi  huo utakao anza mwezi  Septemba mwaka 2026  ukiwa na madhumuni  ya ushirikiano  katika kupambana dhidi ya usafirishaji  haramu wa binadamu  ambao ni kosa linalovuka mipaka.

"Manusura  wakubwa wa usafirishaji haramu wa binadamu ni makundi ya wasichana na watoto wadogo  ambao wanatumiwa kwa njia ya udanganyifu kwa lengo la  wanaowatumia  kujinufaisha kwa kujipatia fedha hivyo kwa kushirikiana tutaweza kutokomeza"amesema Kisiroti.
Afisa ustawi wa jamii  mkoa wa Shinyanga Lyidia Kwesigabo ambaye amechaguliwa kuwa katibu wa kikosi kazi amesema wamekutana na kujengewa uwezo wa  kupambana na usafirishaji haramu wa binadamu  ambapo lengo lililofanyika ni kutengeneza mpango kazi  na namna  gani kila mmoja kama mjumbe kupambana kupitia mpango kazi unavyojieleza.

Mwajuma Ally kutoka shirika la Community of Volunteers  for the  World ( CVM) kupitia Mradi wa emPoWeReD  II wa  kushirikiana  na Apartnership  with Africa (APA)  na wizara ya Mambo ya  Ndani  kupitia Sekretarieti ya kupinga usafirishaji haramu wa binadamu (ATS)  na  kwa mkoa wa Shinyanga wapo kwaajili ya kutengeneza kikosi kazi cha kupinga usafirishaji haramu wa binadamu .

"Tumefanya makubaliano na kuunda kikosi kazi cha mkoa wa Shinyanga  ambacho kinakwenda kutoa  elimu ya uelewa maeneo mbalimbali ikiwemo shuleni na kwenye jamii  pia tumekuwa tukishirikiana na  Chama Cha Wafanyakazi wa Hifadhi ,Hoteli,Majumbani, na Huduma  za  jamii na Ushauri  (CHODAWU ) nakutoa elimu kwa wasichana wa kazi za nyumbani  " amesema  Mwajuma.

Mwajuma amesema kikosi kazi kitaenda kushirikiana  kwa pamoja katika kutoa elimu kwa jamii,kutambua viashiria vya usafirishaji  haramu wa binadamu,kuzuia  na kuwasaidia  manusura  kupata msaada stahiki  .

Afisa Sheria kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani  Sekretarieti ya kuzuia na kupambana na usafirishaji haramu wa binadamu Providence Simbila  ambaye alikuwa mwezeshaji wa kikao hicho amesema  wamefanya kazi  ya kutengeneza kikosi kasi kwa kuweka wadau mbalimbali.

"Katika kikosi hicho  wataweza kuripoti  yale yaliyobainika kwa utaratibu ulioonyeshwa kwenye mpango kazi wao  na  sio kuanzisha shughuli  mpya ambapo wataitafanya kwa  kujumuisha  shughuli za kila siku wanazoendelea nazo kuzifanya" amesema Simbila.

Kikosi kilichoundwa kinajumuisha wadau kama ofisa uhamiaji. jeshi la polisi, Mwendesha mashitaka ,hakimu mkazi,ustawi wa jamii,Maendeleo ya jamii, mganga mkuu wa mkoa,Afisa kazi ,kiongozi wa dini na mwandishi  wa habari.

Post a Comment

0 Comments