WILAYA ya Kahama mkoani Shinyanga imejivunia kuongezeka kwa maendeleo kwa kasi kutokana na serikali ya awamu ya sita kuleta zaidi ya shilingi bilioni 295.2 fedha za utekelezaji miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Mkinda amesema hayo leo wakati wa kutoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha kuanzia mwezi Novemba 2025 hadi Juni 2026 kwenye Halmashauri Kuu ya Chama Wilaya hiyo.
Mkinda amesema kupitia fedha hizo upande wa sekta ya afya wilaya ilipokea zaidi ya shilingi bilioni kumi kwaajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya vituo vya kutolea huduma za afya na kuwezesha utekelezaji wa ujenzi wa jengo la mama na mtoto,jengo la bima,ujenzi wa mtambo wa kuzalishia hewa ya oksjeni na jengo la uraibu wa madawa Manispaa ya Kahama.
“ kuna ongezeko ujenzi wa nyumba tano za watumishi katika vituo vya afya Nyalwelwe,Chambo na Butibu halmashauri ya Ushetu na ongezeko la upatikanaji wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi katika vituo vya kutolea huduma za afya wilaya nzima kutoka asilimia 76 hadi kufikia asilimia 88”.amesema Mkinda.
Ameongeza "kuna uendelezaji wa ujenzi wa vituo vitano vya afya vya Bulige na Mwalugulu halmashauri ya Msalala".
Mkinda
amesema wamepokea watumishi 142 wa ajira
mpya hivyo kuwa na ongezeko la watumishi 406 kutoka 1,104 wa awali nakufika
watumishi 1,510.
Mwenyekiti wa chama hicho Thomasi Myonga amesema kuna kata 58 na serikali imeendelea kuleta fedha nanyi mmejionea sio kitu cha siri hivyo kumuombea kwa mungu ili aendelee kutekeleza na kufikia mwisho wa uongozi wake.
“Sasa hivi watoto wanaenda shule,kina mama wanajifungua,kilimo na mifugo kinasimamiwa vizuri hivyo changamoto kila kitu kikifanyika kinaibuka lakini zote zinaendelea kutatuliwa ikiwemo utolewaji wa ajira hivyo chama kiendelee kudumu”amesema Myonga.
Myonga amempongeza mkuu wa wilaya kwa wasilisho la taarifa ambapo ameshirikiana na wabunge wa majimbo na zipo changamoto ambazo madiwani wanatakiwa wazifuate mfano wachimbaji wa madini vijana maeneo yenye machimbo hawaunganishwi kupata leseni kwani wanapata watu kutoka maeneo mengine
“Tutataka kuona vijana wangapi wa Wilaya ya Kahama wanachimba na wamepewa leseni ambapo viongozi wanao uwezo wa kuwashika mkono vijana ili baadaye wakinufaika waje kuwakumbuka”amesema Myonga..
Hata hivyo
katibu wa chama wilaya ya Kahama Andrew Chatwanga ameeleza wapo wenyeviti ambao wamekuwa hawafanyi mikutano wala madiwani hawafanyi kwa kuogopa kuulizwa maswali lakini ushauri
itisheni mikutano muwaeleze wananchi kinachotekelezwa ili kupunguze maswali.



0 Comments