MADIWANI USHETU WAKUMBUSHIA MGAWANYO WA MALI ZA HALMASHAURI

MADIWANI wa Halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wameomba   mgawanyo wa mali zao zilizobaki Kahama mjini  baada ya halmashauri  ya ushetu kuhama na  kuomba pia makampuni  waliyofunga nayo mkataba kulipa madeni wanayodaiwa zaidi ya shilingi  bilioni 1.1   na ushuru baada ya kufikia  kikomo kwa mwaka wa fedha 2025/2026

 Baadhi ya Madiwani wamesema hayo leo  kwenye kikao maalum cha  baraza la madiwani  kilichohusu   ufungaji wa hesabu za Hamashauri kwa mwaka  wa fedha 2025/2026  ambapo walihoji   utolewe  ufafanuzi zaidi juu ya mgawanyo wa mali.

Diwani  Ester Matone amesema  wakati ilikuwa ikisomeka halmashauri  moja  ya Msalala,Kahama na Ushetu  waligawana mali na waliziacha eneo la Manispaa ya Kahama chakushangaza  mali za ushetu hawajapewa na  bado wanaona kuendelea kuwepo mgogoro.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Gagi Lala amesema   suala la majengo  kugawanywa limekuwa  likiumiza kichwa  kwani ameliomba mno  kwenye mamlala mara kwa mara  kutokana na majibu ya viongozi aliwaomba madiwani wawe na subira huenda litafika  mwisho.

"Kaimu mweka hazina wa Halmashauri hiyo  Charles  Matuba akisoma  taarifa kwenye kikao hicho amesema  halmashauri  hiyo ina mali  za kudumu  ya shilingi bilion 40 .9  na kunamchanganuo wake isipokuwa mali ambazo zinapaswa kugawanywa zilizopo Manispaa ya Kahama ambazo zitakuja kwwnye taaeifa yake

Kaimu  Katibu tawala Mkoa wa Shinyanga  Ibrahim Makana  alikiri  kutambua mgogoro  wa mali kati ya Halmashauri ya Ushetu na Kahama  jambo limefikia pazuri  kwani lilipelekwa kwa mwanasheria Mkuu wa Serikali  na kulitolea majibu  kwa maandishi  hivyo aliahidi  majibu yaliyotolewa kuyawasilisha  kwa barua baraza la madiwani  lijalo.

"Naipongeza Halmashauri ya Ushetu kwa usimamizi mzuri wa fedha za miradi na mali za umma hivyo mkurugenzi aendelee kulea vyema wafungaji wa fedha za serikali na elimu hii ilisishane ili wataalamu waendelee kufanya kazi nzuri"amesema  Makana.

 Makana amesema  kuhusu Makampuni yanayokwrpa kulipa ushuru wa huduma kwenye Halmashauri aliomba kuorozeshwa makampuni yote yanayodaiwa ili kuyaweka pamoja mkoa mzima na

Post a Comment

0 Comments