Na Kareny
Masasy,Shinyanga
IDARA ya uhamiaji mkoa wa Shinyanga imeeleza wapo baadhi ya watu ambao wamekuwa wakichukua hati ya kusafiria (paspoti) kisheria kabisa lakini wakifika mpakani hawazionyeshi na badala yake wanakamatwa kwa kosa la kutumia njia za panya kusafiri.
Hayo yamesemwa na Mrakibu wa Uhamiaji kutoka mkoani Shinyanga Issa Kisiroti alipokuwa akitoa elimu juu ya uhamiaji salama kwa kutumia njia zilizo halali kisheria katika semina iliyotolewa na shirika la CVM and APA kwenye Mradi wa emPoWeReD II kwa kushirikiana na Chodawu, Wote sawa chini ya ufadhlili wa shirika la Kimataifa la Italian Agency for Development Cooperation kwa maafisa wa serikali kutoka idara tofauti tofauti.
Kisiroti
amesema sheria ya Uhamijai inaeleza
lazima ukikata hati ya kusafiria upite kwenye mipaka wakati wa kwenda na
kurudi lakini wapo ambao wamekuwa
wakikeuka sheria hiyo na pindi mtu
akikamatwa atachukuliwa kama mtu anayefanya biashara ya magendo.
“Idara ya
Uhamiaji tumekuwa tukitoa elimu kwenye
kila kata kupitia kampeni ya Mjue
jirani yako ambapo tunawaeleza
mtu wasiyemfahamu watatakiwa
wamtambue nakutoa taarifa ili hatua za
kisheria zichukuliwe” amesema Kisiroti.
Kisiroti amesema wapo baadhi ya maafisa siyo waadilifu wamekuwa wakiungana na watu wanaofanya biashara
za magendo ya kusafirisha binadamu nakuwasindikiza kuwatoa mpakani wakati huo wanapewa fedha (hongo) hilo nalo ni
kosa kisheria.
“Tanzania imekuwa ikipokea wahamiaji
haramu wengi ambao kutoka nchi za Kongo,Burundi na Rwanda wakitumia njia zisizo halali lakini wamekuwa wakikamatwa na kupewa
elimu na kadri siku zinavyokwenda wahamiaji haramu wanondoka sababu wanakuwa na uelewa
wa kukata hati ya kusafairia hata ya muda mfupi”amesema Kisiroti.
Kaimu
kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga
Rafael Msela alipokuwa mgeni
rasmi kwenye semina hiyo alisema maafisa
wote waendelee kuwa mabalozi wa
kupinga usafirishaji haramu
wa binadamu nakutoa elimu kwa
jamii kuhusu viashiria vya usafirishaji
haramu.
“Napenda
kutoa ombi na wito kwa wadau wote
serikalini,vyombo vya ulinzi na usalama
,mahakama,ofisi ya mashtaka,asasi za kiraia ,taasisi za dini , vyombo vya
habari na washirika
wa maendeleo kuendelea
kuimarisha ushirikiano wa pamoja”amesema Msela.
Mwezeshaji kwenye semina hiyo kutoa wizara ya mambo ya ndani Providence Simbila amesema
kusafirisha sio kosa bali matendo ya kuwasafirisha kinyume cha sheria ndio kosa ambalo mtu anakamatwa nalo na faini yake nikifungo cha kuanzia miaka mitatu nakuendelea au fedha.

Mwezeshaji wa Mradi huo kutoka CVM Mwajuma Ally alisema Mradi utadumu kwa kipindi cha miaka mitatu ambapo umeanza rasmi mwaka 2026 hivyo utakuwa na utekelezaji wa shughuli mbalimbali kuhakikisha usafirishaji haramu wa binadamu na wafanyakazi wa nyumbani wachukuliwa kwa kufuata sheria




.png)

.png)





0 Comments