VIKUNDI VYA WAJASIRIAMALI WADOGO KWENDA KUONYESHA BIDHAA ZAO MAONYESHO YA 50 JIJINI DAR-ES-SALAAM


Na Kareny  Masasy,Shinyanga 

VIKUNDI  vya wajasiriamali   wadogo  mkoani Shinyanga  vinavyojishughulisha na usindikaji wa mazao  nakuongeza mnyororo wa thamani  vimewekwa  kwenye orodha ya maonyesha ya kitaifa ya biashara  jijini Dar-es-salaam  mwaka huu.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita amesema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari  ambapo alieleza vikundi  vilivyo tayari mpaka sasa ni vitatu ambavyo vyote  vilipata  mkopo wa asilimia kumi kutoka halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama.

Mhita amesema   mkoa ulishiriki mwaka jana maonyesho hayo ya biashara  jijini Dar-es-salaam  na kubahatika kupeleka  vikundi viwili vinavyosindika mazao kama mchele ambapo walinufaika na kuuza wote kabla ya maonyesho hayajaisha.

“Wafanyabiashara wakubwa,wakati na wadogo  ikiwemo wachimbaji wa madini watahudhuria  maonyesho ya 50 ya biashara wakitokea mkoani Shinyanga  kwani lengo  kuona wengine wanafanya  nini nakutangaza fursa  za biashara zao ndani nan je ya nchi” amesema  Mhita.

 Mhita amesema  mkoa wa Shinyanga una fursa nyingi za kiuchumi na ukiangalia   upande wa kilimo kuna zao la Tumbaku,Pamba,Mpunga na Choroko  ambayo yanalimwa  sana  na   wapo wafugaji wanaofuga mifugo kwa wingi.

Upande wa wachimbaji wadogo nao  wameanza kukopesheka  hivyo kuna wachimbaji wanawake na vijana ambao wakipata fursa ya kwenda kuonyesha  biashara na  shughuli zao watajitangaza  kwaajili ya kupata fursa za masoko.

Ofisa biashara  mkoa wa Shinyanga Magreth  Warioba amesema  maandalizi  wameyafanya kikamilifu kwaajili ya maonyesho ya kitaifa  na viwanda vikubwa vitatu vitashiriki .

Warioba amesema  serikali imekuwa bega kwa bega  kuwawezesha wajasiriamali  kuwekeza kwenye uchumi  baada ya kupatiwa  mikopo ya asilimia kumi kutoka mapato ya kwenye halmashauri.


Post a Comment

0 Comments