Na Mwandishi wetu,Kahama WAKAZI
wa nchi tano za ukanda wa Afrika Mashariki wameanza kunufaika na
uwepo wa bidhaa zinazotengenezwa na kiwanda cha Musumba Steel
kilichopo Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga.
Hayo
yamesemwa leo na Mkurugenzi wa kiwanda hicho Albert Uwiragire
alipokuwa akiongea na waandishi wa habari waliotembelea kwenye kiwanda
hicho kilichopo eneo la Viwandani Chapulwa kata ya Mwendakulima. Uwiragire
amesema kiwanda hicho kilianza rasmi mwaka 2023 na kuzalisha
bidhaa za mabati ya aina mbalimbali ,misumari na vyuma vya mabomba
kwaajili ya kutengeneza Milango ya geti na Madirisha.
Uwiragire
amesema uwepo wa kiwanda hicho kwa Manispaa ya Kahama imekuwa ni
karibu kwani wateja kutoka nchi za Kongo,Rwanda,Burundi ,Uganda
ikiwemo Mikoa ya Tanzania wataweza kunufaika zaidi kwa bidhaa hizi
ambapo usafirishaji utatumia zaidi njia ya reli ya kisasa (SGR) kwa
kituo cha bandari kavu kilichopo Isaka.
Uwiragire
amesema wateja wamekuwa wakija kutoka kwenye maeneo hayo ambao kabla
ya kuanza kiwanda hicho walilazimika kusafiri kwenda Dar-es-Salaam
chukua bidhaa nakutumia muda mrefu tofauti na wakija Kahama ni muda
mfupi.
"Kiwanda hiki
kimeweza kusaidia serikali kutoa ajira kwa vijana nakusaidia familia
zao hivyo tunamshukuru Rais Samia Suluhu kurahisisha mazingira ya
uwekezaji na Mkuu wa Mkoa kutupokea vizuri kwa kushirikiana na ofisi ya
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga kutuonyesha eneo lingine la
kuongeza kiwanda hiki ili shughuli za kiwanda ziweze kuwa endelevu
zaidi kwenye uzalishaji"amesema.
Uwiragire
amesema matarajio yao kuwekeza kwenye kiwanda kwani wanatengeneza
bidhaa nyingi ambazo hata mtu mwenye uwezo wa hali ya chini anaweza
kumudu kununua na kwenda kwenye maonyesho ya 50 ya biashara ya Taifa
jijini Dar-es-Salaam ni fursa kwao na wateja wanaohitaji bidhaa
zinazotoka kwao Meneja
wa Kiwanda hicho Halfani Kareem amesema tangu kianzishwe wameweza
kupata wateja wa hapa nchini zaidi kutoka kanda ya ziwa,kati na
Magharibi changamoto ilikuwa upatikanaji bidhaa kwa urahisi kwenye
mikoa ya kanda hizo.
Kareem
amesema tayari wametoa ajira kwa watu 65 ya muda mfupi naya kudumu
ikiwa kazi zikipungua wanabaki watu 20 wenye ajira ya kudumu na serikali
imekuwa ikipata mapato yake kupitia kodi wanazolipa na mpango uliopo
kuanzisha bidhaa zingine kama nondo na vyuma vya kuchomelea (Welding
Electronic).
"Tunataka
kwenda kwenye maonyesho ya biashara ya 50 kwa kuonyesha bidhaa zetu ili
watu wafahamu viwanda haviko mkoa wa Pwani pekee bali hata mkoa wa
Shinyanga una kiwanda kinachozalisha bidhaa kuhimu"amesema Kareem.
|
0 Comments