Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa ccm wilaya ya Shinyanga vijijini
Edward Alex akimtunuku hati ya heshima mbunge wa jimbo la SolwaMh Ahamed Salum kwa mchango wake mkubwa wa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM kwa kuchangia shughuli za maendeleo kwa wananchi wa jimbo la
Solwa.
Mwenyekiti huyo alisema mbunge Salum ni tofauti na wabunge
waliopita kwenye jimbo hilo kwa kuchangia shughuli za maendeleo.
Ambapo katika mfano aliouonyesha ni kutoa magari ya wagonjwa nane katika vituo vya afya na zahanati mbalimbali zilizomo kwenye kata hiyo,licha ya mchango huo, amesema kuwa wananchi wenyewe ni mashahidi ambapo katika ujenzi wa mabweni hasa zahanati amekuwa akitoa mifuko 200 ya saruji kwa lengo la kufikia hatua ya lenta bila kushirikisha michango ya wananchi kwenye ujenzi na kisha halmashauri kukamilisha ujenzi huo,
Hata hivyo licha ya kutunikiwa cheti wananchi wa jimbo hilo wamekuwa wakimpa pongezi katika shughuli za kuwaletea maendeleo hasa kwenye upande wa afya amekuwa ni mkombozi mkubwa katika maisha.
Hivi karibuni katika ziara yake ameweza kutoa mifuko ya saruji 200 kwa kila zahanati inayotakiwa kujengwa zikiwemo wodi za wanawake kwenye vijiji na karibu kata zote za jimbo hilo.

0 Comments