WAKAZI wa kitongoji cha Mwabagikulu katika Kjiji cha Ikonongo kata ya Salawe halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji hali ambayo
inawafanya wakazi wa kijiji hicho kuamka nyakati za usiku kutafuta maji huku wakiwa na hofu ya
kuhatarisha maisha yao,ambapo mkazi mmoja wa kijiji hicho Ndelemo
Maguta alisema kuwa inawalazimu kutafuta maji nyakati za usiku sababu
ukienda majira ya mchana hakuna maji huku watu ni wengi,wengine utakuta wanawatuma watoto kwenda kushinda kwenye visima vya maji wakisha jaza huwafuata.
|
0 Comments