WATOTO na akina mama manispaa ya Shinyanga wameandamana kwa lengo la
kupinga ukatili dhidi ya watoto wa kike uliofanywa na kundi la
waharamia wa kiislamu linalojulikana kama boko haramu lililopo
nchini Nigeria mara baada ya kuwateka wanafunzi zaidi ya 270.
Maandamano
hayo yalishirikisha pia shirika lisilo la kiserikali la AMSK
FOUNDATION la mjini Shinyanga linalojihusisha na shughuli za kutetea
ukatili dhidi ya watoto wa kike na akina mama huku mkurugenzi
mtendaji wa shirika hilo Lilian Kowfie akieleza kuwa wameamua kufanya
hivyo ili kukemea vitendo viovu vinavyofanywa kwa watoto wa kike.
Pia
alisema kuwa shirika hilo limeguswa na kusikitishwa juu ya watoto wa
kike waliotekwa huko nchini Nigeria jimbo la Borno mnamo tarehe 15
April mwaka huu ambapo zaidi ya watoto 270 wa shule walitekwa na kundi
la Mgamo la kiislamu Boko Haramu na kupelekwa kusiko julikana kwa madai
kuwa watoto wa kike hawastahili kusoma.
“Tumeamua kuandamana kwa
kushirikiana na wakazi wa mjini shinyanga na viongozi wa madhehebu
mbalimbali ya kidini na serikali ili kukemea vitendo viovu
vinavyofanywa kwa watoto wa kike na kuonekana hawana haki ya kupata
elimu kama watoto wa kiume.”alisema Kowfie.
Kowfie alisema tabia
ya unyanyasaji dhidi ya watoto wakike imedhidi kushika kasi mjini
shinyanga na sehemu nyingine duniani wameona vyema kukemea vitendo
hivyo wakishirikiana na wananchi, viongozi wa serikali na Dini kutoa
elimu kwa wananchi wa mjini humo kuachana na matendo ya kikatili
yakiwemo pia mauaji ya vikongwe.
“Maandamano haya kwajili ya
amani ambayo tunakemea vitendo vya kikatili vinavyofanywa juu ya watoto
wa kike hapa nchini na Afrika kwa ujumla ambapo pia tunashirikiana na
wenzetu wa Nigeria kulaani matendo ya kikatili na kulitaka kundi la
Boko Haramu kuwaachia watoto hao iliwaendelee na masomo yao” alisema
Kowfie.
Naye mkuu wa wilaya ya Shinyanga AnnaRose Nyamubi
aliwataka wakazi wa mjini humo kuacha kuendekeza mila potofu zilizopitwa
na wakati kwa kuacha kuwasomesha watoto wa kike na kuwapeleka kwenye
machungo huku wengine wakiozeshwa wakiwa na umri mdogo.
Nyamubi
alisema tatizo la mkoa wa shinyanga ambalo lenye idadi kubwa la kabila
la wasukuma wamekuwa wakiendekeza mila na desturi za mababu zao za
kutowasomesha watoto wakike wakiamini watoto hao ni wakuolewa na
hawawezi kuleta maendeleo, na kusema kuwa mila hizo zinafaa kupingwa
vikali.
0 Comments