MRADI
wa mbwawa la umwagiliaji katika kijiji cha Ishololo kata ya Usule
halmashauri ya wilaya Shinyanga umeingia sura mpya mara
baada ya naibu waziri wa kilimo,chakula na ushirika
Godfrey Zambi kuutembelea na kujionea hali halisi
ya kutokamilika kwake ingawa mkandarasi ameongezewa
muda huku akisikitishwa na uongozi ngazi ya kanda,mkoa na
wilaya kutoshirikishwa na kuutambua.
“Nina kiri baadhi ya miradi imetumia fedha nyingi zaidi ya
shilingi million 200 lakini miradi hiyo imefanywa vibaya ,pia
serikali ilidhamiria kuweka mradi huu hapa hali imeonekana
mkandarasi ndio hovyo na kutokuwa na uwazi kwenye mradi,
ikiwa uongozi wa ngazi mbalimbali unaotegemewa haujashirikishwa.”alisema Zambi.
Ambapo waziri huyo mara baada ya kujionea alipewa maelezo na
injia wa skimu ya umwagiliaji Godrey Mbwambo kuwa mkataba wa
mradi huo ulifungwa tarehe 15/02/2013 kati ya katibu mkuu na wizara ya kilimo
chakula na ushirika na mkandarasi aitwaye SYSCON BUILDERS wa jijini
Dar-es-salaam chini ya mhandisi mshauri CODA AND PARTERS ya Kenya
baada ya kufunga mkataba mkandarasi alitakiwa kuanza kazi mwezi mmoja
baada ya kufunga mkataba huo.
Mbwambo alisema kuwa mradi huo ulilenga kuwanufaisha
wakulima na wafugaji kutoka vijiji viwili vya Ishololo na
Tindeng’hulu ambao ungeweza kunufaisha wakulima zaidi ya 1500 na
kiasi cha hekta zipatazo 500 zingeweza kumgwagiliwa na maji kutoka
katika bwawa hilo.
“Mradi huu ambao unafadhiliwa na mradi wa uwekezaji katika sekta ya
kilimo wilaya (DASIP) imechangia kiasi cha zaidi ya shilingi millioni
740 na mfuko wa umwagiliaji (DIDF) kwenye mradi huo imechangia kiasi cha
shilingi millioni 200 na kufanya jumla ya gharama ya mradi ya
shilingi millioni 940”alisema Mbwambo.
Pamoja na maelezo hayo naibu waziri huyo alitaka kupata majibu kutoka
ofisi ya kanda ambao walidaiwa kuwa wahusika wa mradi huu,pia
alisema kushindwa kutekelezeka fedha hiyo ninavyofahamu
itarudi benki ya Afrika (AFDB) kwa kuwa mradi wa DASIP uliisha muda
wake 31/12/2013, ingawa inaelezwa aliongezewa muda na kushindwa kukamilisha
pia.
Zambi alisema kuwa kweli katibu wa wizara ndio aliyesaini mikataba
yote hivyo yatahitajika mazungumzo ofisini,,ikiwa mhandisi wa
umwagiliaji kutoka ofisi ya kanda ya ziwa iliyopo jijini Mwanza Ebeneza Kombe
alisema kuwa mradi huo uliandikiwa jumla ya shilingi billion 1.2
katika bajeti yake ya mwaka 2013 lakini hazikuja katika ofisi
hizo ililazimu tena kuandika maandiko mengine kwa kuanza
upya.
Hata hivyo mbunge viti maalum Azzah Hilali alimueleza naibu waziri
kuwa ofisi ya kanda wanyooshe maelezo mradi huo wao
kama halmashauri na mkoa walielezwa hawahusiki bali ni ofisi ya kanda na wizara
ikiwa wakulima wamekuwa wakilalamika kushindwa kutekelezeka kwa wakati
huku mkandarasi hana vifaa matokeao yake kufanya shughuli zake binafsi vijijini
hapo.
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Mohamed Kiyungi alisema kuwa kiasi cha
shilingi millioni 200 zilizotoka DIDF na kuhamishiwa akaunti ya
mradi wa DASIP Mwanza wao kama halmashauri walikuwa wanaomba fedha
hizo zirudishwe kwenye akaunti ya halmashauri ili ziweze kuendeleza shughuli za
miradi ya umwagiliaji.
Diwani wa kata hiyo Amina Bundala alisema kuwa alitakiwa kuanza kazi
tarehe 15/03/2013 na kazi hii ilitakiwa ifanyike ndani ya siku 240 sawa na
miezi nane ,licha ya kuongezewa muda sisi viongozi tumeonekana
waongo sababu tangu mwezi huo mifugo inakunywa matope badala ya
maji wakulima wamevurugiwa mashamba yao ikiwa bwawa hilo linahitaji
kuhudumia kata za Bukene,Imesela Usule na Tindenhulu.
Mradi huu uliibuliwa na wananchi wenyewe katika bajeti ya kijiji ya mwaka
2011/12 kwa kutaka bwawa kwaajili ya kilimo cha umwagiliaji kwa zao
la mpunga ikiwa walikuwa wakikosa maji ya kutosha kwa kuliendeleza zao
hilo na kupata mavuno ya kutosha huku halmashauri ikipata pato la
ndani zaidi kupitia ushuru za zao la mpunga.
0 Comments