CHANGAMOTO
kubwa inayowakumba watoto waliochini ya umri wa miaka mitano kiafya
ni upungufu wa damu na ugonjwa wa malaria hali ambayo inapekekea kuleta
msongamano wa wagonjwa katika kituo cha afya kilichopo kata ya
Iselamagazi tarafa ya Nindo wilayani Shinyanga.
Akiongea na
waandishi wa habari waliokuwa wametembelea katika kituo hicho mganga
mkuu wa Dkt Heleni Kaunda aliwaeleza kuwa msongamano wa wagonjwa pia
unaletwa kwa kuhudumia wagonjwa ambao wanahitaji matibabu zaidi kutoka
zahanati sita zinazozunguka kata hiyo.
Dkt Kaunda alibainisha
kuwa watoto waliochini ya umri wa miaka mitano zaidi ndio wamekuwa
wakipata ugonjwa wa malaria ya homa kali pamoja na upungufu wa damu hali
ambayo inaleta msongamano ikiwemo kuhudumia kwa masaa 24.
“Msongamano
wa wagonjwa upo,wengi wamekuwa wakipelekwa rufaa kwa malaria kali na
upungufu wa damu ikiwa zaidi watoto kwa siku wawili mpaka wanne,
pamoja na akina mama wanaoshindwa kujifungua “alisema Dkt Heleni.
Pia
Shija Ramadhani mkazi wa kijiji cha Iselamagazi alionekana kuhudhuria
katika hospitali ya mkoa huku akiwa amembeba mtoto wake mgongoni baada
ya kuulizwa na mwandishi alidai kuwa mtoto huyo alilazwa katika kituo
cha afya lakini hali ilionekana kuwa mbaya kutokana na kutopatiwa dawa
tangu alazwe.
Naye afisa mtendaji wa kata Paul Kulwa alisema
kuwa kata ya Iselamagazi inazahanati mbili ambazo zipo katika vijiji
vya Mwamakaranga na Homango ambapo inahudumia zaidi ya vijiji sita
pamoja na kata ya Lyabusalu mpya yenye vijiji saba ikiwemo vijiji vya
jirani ya wilaya ya Kishapu na mkoa wa Mwanza.
Hata hivyo alisema
kuwa kata hiyo inaidadi ya watu zaidi ya 20,000 vituo vya kutolea
huduma ya afya vichache na upatikanaji wa dawa unakuwa wa shida kwani
huja chache ambazo hazitoshelezi idadi ya watu waliopo na wanaotoka
nje ya kata hiyo.
Aidha baadhi ya wananchi wa kijiji cha
Mwamakaranga Rafael Paul na shija Masalu walisema kuwa upatikanaji wa
huduma umekuwa shida ziku zote kutokana na msongamano wa wagonjwa katika
zahanati na kituo cha afya ikiwemo kukosa madawa hivyo hulazimika
kwenda kununua dawa.
Changamoto hiyo imetokana na zahanati pamoja
na vituo vya afya hasa vijijini kutokuwa nadawa hata kama zikiletwa
hazikidhi matakwa ya idadi ya watu waliopo kwenye eneo husika
,ambapo jamii huamua kwenda kununua kwenye maduka binafsi huku zingine
zikiwa feki.
Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dtk Fredrick
Mlekwa alisema kuwa kweli wagonjwa wanaotoka nje walio wengi ni kutoka
maeneo ya vijijini,wakifika hapa wanakuwa na hali mbaya kiafya hiyo
inatokana na uelewa mdogo wa wananchi hao au huduma zinazotolewa katika
vituo vya afya na zahanati pamoja na za watu binafis kuwa na kiwango
kisichokidhi kiafya kwa kujali maslahi yao.
Naye mkuu wa mkoa wa
Shinyanga Ally Rufunga alisema kuwa mkoa huu umetenga jumla ya
shilingi billion 3.5 kwaajili ya kukabiliana na changamoto mbalimbali
za kupata afya bora katika jamii ambapo mpaka sasa ni asilimia 70 ya
vituo vya afya na zahanati ni asilimia 60 huku halmashauri mbili zikiwa
na hosptal.
0 Comments