MAHAKAMA ya hakimu mkazi wilaya ya Shinyanga imewahukumu wakazi wawili
wa kijiji cha Shatimba wilaya ya shinyanga mkoani hapa kwenda jela
kwa miaka 242 baada ya kupatikana na makosa matatu ambayo ni ubakaji ,
wizi wa kutumia silaha na kujeruhi.
Waliohukumiwa ni Mathias
Kaloga (40) Jamesi Moshi (35) wote wakiwa wakazi wa kijiji hicho na
kutenda makosa hayo October 10, 2012.ambapo walivamia nyumbani kwa
malamikaji wa kwanza Tesha Jidomela wakiwa na bunduki na mapanga
,walimjeruhi na kuiba simu tatu za mkononi.
Akiendesha mashitaka
hayo jana katika mahakama ya wilaya ya shinyanga mwanasheria wa serikali
Salome mbuguni aliambia mahakama hiyo kuwa baada ya washitakiwa hao
kufanikiwa zoezi la kupora mali hizo ambapo pia waliwabaka wake za
walalamikaji kwa kubadilishana zamu kwa zamu.
Pia usiku huohuo
walivamia katika mji mwingine wa Sai Jidomela ambaye ni mdogo wake wa
mlalamikaji namba moja walivamia kwa silaha hizohizo na kufanikiwa
kupora simu moja ya mkononi na kisha kuondoka na sh, elfu 57 ambazo
zilikuwa kwenye mfuko wa suruali yake.
Mbuguni alisema kosa la
kwanza la kuiba kwa kutumia silaha kila mshitakiwa atatumikia jela miaka
60 kutokana na kuvamia sehemu mbili ,ambapo shemu ya kwanza ni miaka 30
kwa kila mmoja, kutokana na kifungu cha sheria no.287 (a)16 cha kanuni
ya adhabu, kuvamia na kujeruhi ambapo ni kinyume cha sheria no.225(a)44
kila mtuhumia ni miaka 2,na kulipa faini ya laki mbili.
Aliongeza
kuwa kosa la kushambulia,kuzuru na kubaka ni kinyume cha sheria namba
241 kifungu cha 16 ambapo watuhumiwa wote wanatakiwa kutumikia jela
miaka 60 kwa kila mmoja kutokana na kuwabaka wake wa walalamikaji wote
wawili kwa zamuzamu.
Akitoa hukumu hiyo hakimu mkazi wa mahakama
ya wilaya ya shinyanga Thomsoni Mtani alisema kuwa kutokana na mashitaka
hayo mtuhumiwa wa kwanza atatumikia jela miaka 122 na mtuhumiwa wa pili
atatumikia jela miaka 120, jumla ya miaka yote ni 242, pamoja na
viboko kumi na mbili kwa kila mmoja kuingia na kutoka.
0 Comments