MAHAKAMA
kuu kanda ya Tabora imeanza kusikiliza kesi za mauaji mbalimbali
katika mkoa wa Shinyanga kwa mwaka huu ikiwa kesi kumi na moja
zitasikilizwa ndani ya mwezi mmoja ikiwemo mauaji yanayotokana na imani
za kishirikina.
Ambapo mara baada ya kumalizika ufunguzi wa kusikiliza kesi hizo
mahakama ilianza kwa kuangalia upande wa mtuhumiwa Mbula Mako
aliyekuwa mganga wa kienyeji kufanya mauaji dhidi ya kikongwe Buguta
Mashilima huko katika kijiji cha Nobora wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Kesi
hiyo iliendeshwa na jaji Haruna Songoro huku akisema kuwa mkoa wa
Shinyanga na Simiyu unakesi nyingi ambapo jumla ya kesi 11 za mauaji
zitasikilizwa kwa kipindi cha mwezi mmoja.
Katika
ufunguzi uliozinduliwa na jaji Songoro kwa kusikiliza kesi za mauaji
mbalimbali Siku ya kwanza ya kuendesha kikao kulifanyika usikilizwaji
wa kesi moja ya mauaji yaliodaiwa kutokea kwa imani potofu za
ushirikina.
Kwa upande wa mashitaka
mtuhumiwa alitenda mauaji hayo mnamo novemba 21 ,2011 kijiji cha nobora
bariadi majira ya usiku baada ya kumtumbikiza kisimani marehemu
ambaye alikuwa bibi yake.
Hata
hivyo changamoto kubwa katika mahakama ya mkoa wa Shinyanga imedaiwa
kuwepo mrundikano wa kesi mbalimbali zikiwemo za mauaji ya vikongwe kwa
imani za kishirikina ambazo hazijasikilizwa na kutolewa hukumu.
Naye
hakimu mkazi mwandamizi mfawidhi mkoa wa shinyanga John Meseka Chaba
ameiomba serikali hapa nchini kupitia ofisi ya mkuu wa mkoa shinyanga
kukamilisha ujenzi wa jengo la mahakama kuu kanda ya ziwa linalojengwa
mkoani hapa ilikurahisisha uendeshaji wa kesi hali ambayo itasaidia kesi
nyingi kusikilzwa kwa wakati
“Endapo
jengo la mahakama ya Rufaa kanda ya ziwa mkoani hapa litakapokamilika
litasaidia kuepusha mrundikano wa kesi mahakamani kwani kesi nyingi
hupangiwa tarehe kila mara kutokana na uhaba wa majengo ya mahakama
kuendeshea kesi hizo pamoja na upungufu wa mahakimu kwani kesi nyingine
zinakuwa hazijamaliza upelelezi”alisema
Chaba
0 Comments